BAADA ya misukosuko ya kupanda na kushuka kwa
matukio mengi, tayari mchakamchaka wa 2017 umeanza, katika burudani ya
kizazi kipya mwishoni mwa mwaka uliopita msanii Darassa ndiye alikuwa
habari ya mjini.
Miezi 12 iliyopita tulishuhudia matukio mengi ya kujiongezea umaarufu
‘kiki’ ya aina tofauti huku yale ya watu maarufu hasa wasanii kuandikwa
na kuzungumzwa kwa wingi kutokana na maisha yao ya kimapenzi nayo
yalipata nafasi kubwa.
Ukiachana na Diamond na Zari ambao uhusiano wao ulikuwa gumzo kama
ilivyokuwa kwa mastaa kadhaa wakiwemo Jux na Vanessa Mdee, msanii wa
Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole au Shishi Baby’naye hakuwa nyuma
katika upande huo.
Shilole akiwa na mpenzi wake wa sasa Boy Caro.
Shilole, 28, ambaye alianza kutamba katika maigizo kabla ya baadaye
kuegemea zaidi katika muziki, ni mama wa mabinti wawili, Joyce na Rahma.
Joyce ndiye wa kwanza na inaelezwa kuwa anaelekea kutimiza umri wa
miaka 14, huku Rahma akitarajiwa kutimiza umri wa miaka 10 baadaye mwaka
huu.
Pamoja na hali hiyo, ndani ya miaka mitatu iliyopita Shilole amekuwa
akitajwa kuhusishwa kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na wanaume kadhaa.
Akiwaza jambo.
Licha ya mwenyewe kukiri kuwa aliwahi kuingiliwa kinguvu na mwanaume
wakati akiwa na umri wa miaka 15, bado inaonyesha hajaamua kuondoa
‘jinamizi’ la mapenzi linalomuandama.
Mwaka 2013, uhusiano wake na aliyekuwa chipukizi wa Bongo Fleva, Ally
Timbulo ulizungumzwa na wengi lakini baadaye wawili hao walivurugana
kisha Timbulo akatua kwa staa wa Bongo Movie, Jacqueline Pentezel ‘Jack
Chuzi’. Mahaba ya Timbulo na Shilole yalidumu kwa zaidi ya miezi sita.
Inadaiwa kuwa baada ya hapo Shilole alikabidhi moyo wake kwa Mbongo
Fleva mwingine, Elias Barnaba ‘Barnaba Classic’, ambaye sasa naye ni
baba wa mtoto mmoja aitwaye Steve aliyezaa na mwanamke mwingine aitwaye
Zuu.
Penzi la Shishi na Barnaba nalo halikuchukua muda mrefu, sababu haikujulikana lakini Barnaba akaamua kuelekeza nguvu kwa mchumba wake wa siku nyingi, mama Steve ambaye ndiye anayeishi naye mpaka sasa.
Kama filamu vile, Shilole akatulia kwa muda kisha akamkabidhi moyo
wake Nurdin Mlawa a.k.a Nuh Mziwanda ambaye aliuchukua moyo huo na
kuusafisha vizuri kisha akamfanya ‘mtoto’ kuwa mtu mwenye furaha kubwa.
Wapenzi hao walionyeshana mahaba yao waziwazi, kuanzia kwenye mitandao,
mitaani, kwenye shoo na hata sehemu nyingine nyingi walikuwa pamoja
wakiongozana.
Shilole akijiachia na mpenzi wake.
Penzi la Shishi na Barnaba nalo halikuchukua muda mrefu, sababu haikujulikana lakini Barnaba akaamua kuelekeza nguvu kwa mchumba wake wa siku nyingi, mama Steve ambaye ndiye anayeishi naye mpaka sasa.
Ikadaiwa kuwa ubabe wa Shilole ukawa kikwazo kwa Nuh ambaye mara
kadhaa aliwahi kupokea vibao vya hapa na pale hadharani kutoka kwa
laazizi wake huyo, baada ya hadithi za wameachana-wamerudiana kutokea
mara kadhaa, mwisho wake wakamwagana rasmi.
Wiki kadhaa baada ya penzi hilo kufa, tetesi zikaibuka kuwa Shishi
Baby ameanguka mikononi mwa dogodogo mwingine, Nedy Music ambaye ni
mwanamuziki wa Bongo Fleva.
Boti ya mapenzi ya wawili hao inadaiwa haikudumu hasa kwa kuwa
haikupata kiki, muda mfupi baadaye Shilole kwa mara nyingine ikaelezwa
kuwa kijana kutoka Tanzania House of Talent (THT), Hamadai kanasa kwenye
penzi la mama wawili huyo.
Watu wa karibu wa wasanii hao wakafunguka kuwa utofauti wa tabia zao ndiyo uliofanya maisha yao ya kuwa penzini kuwa mafupi.
Mwishoni mwa mwaka jana mpaka sasa, Shishi Baby amenasa kwenye mikono ya kijana anayeitwa Adam maarufu kwa jina la Boy Caro.
Wameonekana kuwa pamoja wakiongozana sehemu nyingi, wakipiga picha,
wakifurahia maisha na wamewahi kuhojiwa kwenye kituo kimoja cha redio
hivi karibuni ambapo wakaelezea jinsi wanavyopendana na mipango yao ya
baadaye. Boy Caro siyo msanii ila ni mzoefu wa jiji na anafanya
biashara.
Shishi amechagua maisha yake ya mapenzi yawe sehemu ya umaarufu wake
na ndiyo maana kila anapohama kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine
inakuwa rahisi kujulikana na anaitumia kama sehemu ya kujiongezea kiki.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment