MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari 
Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amesema kuwa japo kuna tetesi zinaenea mtaani 
kwamba amerudiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed 
‘Shilole’ suala hilo halina ukweli wowote ndani yake na wala hafikirii 
kabisa kurudiana na mwanadada huyo.
Tetesi za Nuh kurudiana na Shilole zilianza kuvuma baada ya kusambaa 
kwa kipande cha video kilichowaonesha wakipatanishwa wakati wakiwa 
kwenye safari za Tamasha la Fiesta na watu kujiongeza kuwa wamerudiana.
“Kilichotokea ni kwamba mimi na Shilole tumeondoa tofauti zetu za kibinadamu ambazo tulikuwa nazo baada ya kuachana.
Lakini kuhusu kurudiana hahitakuja kutokea hata siku moja na siwezi 
kurudi nyuma kwenye hili maana nina mpenzi wangu ninayempenda,” alisema 
Nuh.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi












0 comments:
Post a Comment