Mahakama
 ya Mkoa wa Lindi, imemuhukumu kwenda jela miezi nane, Suleiman Mathew 
ambaye alikuwa mpinzani wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na 
Michezo, Nape Nnauye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 katika Jimbo la 
Mtama.
Mathew
 ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Lindi na kiongozi mwenzake 
wa kata wamehukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya
 mkusanyiko bila ya kibali.
Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Mkoa wa Lindi, mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mhina.
Mahakama
 imefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza mashahidi sita wa upande wa 
mashtaka na kujiridhisha kuwa ushahidi wao umethibitika bila kuacha 
shaka.
Waliotiwa
 hatiani na kupewa adhabu hiyo ni Mwenyekiti Chadema mkoani Lindi, 
Selemani Methew pamoja na Katibu wa Tawi la Kata ya Nyangamala, Ismail 
Kupilila.
Akisoma
 hukumu hiyo Hakimu Mhina alisema, upande wa mashtaka ukiongozwa na 
Wakili wa Serikali Juma Maige uliwafikisha mahakamani hapo mashahidi 
sita.
Alisema
 kutokana na ushahidi ulitolewa na mashahidi hao, mahakama imeona upande
 wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao bila 
kuacha shaka yoyote na kuwatia hatiani.
Baada ya kuwatia hatiani mahakama iliwapa nafasi washtakiwa ili waweze kujitetea ambapo waliomba  wapunguziwe adhabu.
Akiwasilisha
 hoja za upande wa utetezi Wakili wa washtakiwa hao,  Deusdet Kamalamo 
aliiomba mahakama isiwape adhabu kali kwa madai kwamba wanafamilia 
inawategemea, hivyo iwapo watapewa adhabu kubwa kutaifanya ikose huduma 
zao.
Baada
 ya utetezi huo, Wakili wa Serikali Juma Maige aliiomba mahakama hiyo 
iwape washtakiwa hao adhabu kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza ili iwe 
fundisho kwao na wengine.
Hakimu
 Mhina akitoa adhabu katika kesi hiyo namba 36/2016, chini ya kifungu 
cha 74 (1) na 75 cha kanuni ya adhabu sura ya 16, alisema mahakama 
inawapa adhabu, kila mshtakiwa  atatumikia kifungo cha miezi minane 
gerezani na kusema nafasi ipo wazi ya kukata rufaa iwapo wataona 
hawakuridhishwa na hukumu hiyo.
Baada
 ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Mathew alisikika akiguna na baadae aliketi
 sakafuni, huku katibu wake wa tawi, Ismail  ambaye alionekana kuchoka 
kutokana na hukumu hiyo akiwa amelowa kwa jasho.
Mahakama
 hiyo pia iliwaachia huru washtakiwa wanne ambao ni wanachama waliokuwa 
wameshtakiwa pamoja na viongozi hao, baada ya ushahidi uliokuwa 
umetolewa na upande wa mashtaka kutokuwa na mashiko ya kuishawishi 
mahakama kuwatia hatiani.
Washtakiwa
 hao ni Bashiru Rashid, Hassani Mchihima, Abdallah Masikini na Mohamedi 
Makolela ambao wote ni wakazi na wakulima wa Kata ya Nyangamala.
Awali
 washtakiwa hao walidaiwa kutenda makosa hayo Aprili 3,  mwaka jana, 
maeneo ya Kata ya Nyangamala, mkoa Lindi, washtakiwa walifanya 
mkusanyiko usio halali.
Akizungumza
 nje ya mahakama hiyo, Wakili wa upande wa utetezi,  Deusde Kamalamo 
alisema wanajiandaa kukata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na mahakama 
hiyo.
“Tutakata rufaa kupinga uamuzi huu, leo naandaa barua ya kuomba nakala ya hukumu ili tuanze kuandaa rufaa ya wateja wangu,” alisema Wakili Kamalamo.
Katika
 Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Methew alikuwa akipambana na Nape ndani ya
 CCM lakini alishindwa kufurukuta katika kura za maoni na baadae 
alijiengua na kujiunga na Chadema na kuwa mgombea ubunge kupitia chama 
hicho.
Katika
 hatua nyingine jana Diwani wa Kata ya Kyangasaga, wilayani Rorya, 
Christopher Kichinda maarufu ‘Protocol’ amehukumiwa kwenda jela miaka 
mitano.
Akizungumzia
 hukumu hiyo Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche, alisema 
diwani huyo alikuwa anakabiliwa na kesi ya Katiba iliyokuwa inamkabili 
kuwa alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya lakini 
alijitoa ambapo mahakama ilimtia hatiani kwa makosa yaliyokuwa 
yanamkabili.
“Ni kilio kingine kwa demokrasia ya nchi yetu na ufanisi kwa siasa za CCM,” alisema Heche.
Mbowe Alaani
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akizungumzia hatua ya Methew kuhukumiwa kwenda jela, alisema huo ni
mkakati ulioandaliwa Serikali ya CCM kudhohofisha upinzani na kuwatisha wasifanye siasa.
Hata
 hivyo, Mbowe aliwagiza viongozi wa chama hicho nchi zima kuandaa orodha
 ya kesi walizonazo ili kuziwasilisha jumuiya za kimataifa kuonyesha 
jinsi upinzani unavyokandamizwa na kupokonywa haki yao ya kufanya siasa.
Alisema Methew amehukumiwa wakati tayari Mbunge wa Kilombero, Peter Lijuakali akiwa ameshahukumiwa kwenda jela miezi sita.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi













0 comments:
Post a Comment