Mahakama
 ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi uliokuwa ukifanywa 
ndani ya nchi ya Tanzania katika kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya 
Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake umekamilika.
Hayo
 yameelezwa na wakili wa Jamuhuri Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi 
Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Hata hivyo Wakili Wilson amedai kuwa huyo bado wanasubiri upelelezi unaofanywa nje ya nchi ambao bado haujakamilika.
Mbali
 na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na 
Sioi Graham Solomon.Wanadaiwa kutenda makosa nane likiwemo la 
utakatishaji wa fedha wa kiasi cha USD milioni sita.
Baada
 ya taarifa hiyo ya upelelezi, Wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba 
mahakama kuwaleza upande wa jamuhuri waeleze hali ya upelelezi ikoje na 
siyo kuleta lugha za ujanja ujanja.
“Tunaomba
 upande Jamuhuri watupe majibu yenye muelekeo, waache lugha za 
ubabaishaji, kama upelelezi haujakamilika waseme basi siyo suala la 
kutueleza umekamilika ndani ya nchi lakini nje bado, haileti maana 
yoyote.”Amesema Magafu.
Akijibu
 hoja hizo,Hakimu Mkeha amesema kitendo cha kesema upelelezi wa ndani 
umekamilika inaonyesha kesi imepiga hatua kwa kiasi fulani hivyo 
ameuagiza upande wa jamuhuri ukija tena ueleze hali ya upelelezi huko 
nje ikoje.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,mwaka huu.
Mbali
 na shtaka la utakatishaji wa fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na 
tuhuma za kula njama, kutoa nyaraka za uongo na kughushi.
Wanadaiwa
 kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi 2013 na 
Septemba 2015 wakati wa mchakato wa Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya 
Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
 











 




 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment