Kikosi cha Stars leo asubuhi kimefanya maziezi yake ya mwisho kuelekea mchezo wake dhidi yaMisri kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2017.
Nahodha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta amesema licha ya mechi ngumu inayowakabili kesho dhidi ya Misri, Stars inataka kuwapa raha mashabiki wake kwenye uwanja wa nyumbani.
“Tunachoangalia sisi ni mechi ya kesho, hatuangalii matokeo finyu au matokeo makubwa. Muhimu ni kushinda mchezo haijalishi kwamba tutaweza kupita au hatutaweza kupita”, amsema Samata ambaye ni mchezaji pekee kwenye kikosi cha taifa anayecheza soka la kulipwa barani Ulaya.
“Hatuwezi kucheza nyumbani halafu tuangalie kama tunanafasi finyu muhimu ni ushindi halafu mambo mengine yatakuja baadaye.”
“Hali ni nzuri, kilakitu kipo sawa wachezaji wana morali na naamini mechi ya kesho itakuwa vizuri”, Samatta alimaliza.
Stars tayari wamemaliza mazoezi yao ya mwisho kulekea mchezo huo na kinachosubiriwa ni keho kuoneshana kazi kwenye uwanaja wa taifa.
0 comments:
Post a Comment