haya ya nguvu za kiume humuathiri mwanaume na mwanamke kwa ujumla. Tatizo hili hulalamikiwa aidha na mwanaume mwenyewe au mwanamke kwa kutofikishwa kileleni na kutofurahia tendo la ndoa, hasa kwa wale walio katika mahusiano.
Zipo sababu nyingi kama
tutakavyokuja kuona lakini matatizo haya humuathiri mtu zaidi
kisaikolojia anapohisi anashindwa kutimiza wajibu wake au mwanamke
kujihisi hapati haki yake ya kufurahia tendo.
Mtu anaweza kuwa na
tatizo dogo ambalo kama ni mshtuko na anapopata mshtuko huo
hujikuta tatizo linazidi hivyo kujikuta mgonjwa yaani ana tatizo.
Kwa hiyo ni vema unapotokewa na
tatizo hili usikimbilie kutumia dawa hasa za asili na hata za
madukani bali waone madaktari wakufanyie uchunguzi katika
hospitali kubwa.
JINSI TATIZO LINAVYOGAWANYIKA
Tatizo la nguvu za kiume limegawanyika katika makundi mawili; Kwanza ni tatizo la kuzidi kwa nguvu za kiume.
Watu wengi wamezoea ukisema tatizo
la nguvu za kiume ni upungufu, lakini lipo hili la kuzidi
isivyo kawaida na kujikuta mtu anashindwa kufikia mwisho au
mshindo, hali hii tutakuja kuiona kwa undani.
Tatizo la pili ni upungufu wa
nguvu, hili ndilo tatizo lililozoeleka sana miongoni mwa wanaume
wengi.
Upungufu wa nguvu za kiume unaweza kuwa mdogo au mkubwa,
nao una sababu zake tutakuja kuziona.
KUZIDI KWA NGUVU ZA KIUME
Hali hii kitaalamu inaitwa ‘Painful
Abnormal Erection of The Penis’. Mwanaume mwenye hali hii
hulalamika maumivu makali ya uume pale unaposimama na hushindwa
kumaliza tendo. Hali hii inaweza kuwa ya muda tu au ikatokea
mara moja moja na wakati mwingine inaweza kuendelea kwa muda
mrefu.
Chanzo cha tatizo hili ni matatizo
au magonjwa ya mfumo wa fahamu, kulazimisha uume usimame kwa
kutumia madawa au njia yoyote ile, uwepo wa mawe katika
kibofu cha mkojo, maambukizi katika njia ya mkojo, maambukizi ya
tezi dume, kuziba kwa mishipa ya damu ya vena inayotoa damu
kwenye uume kurudisha mwilini, na hii huwatokea zaidi wagonjwa
wa siko seli.
Pia matatizo ya mfumo wa damu hasa yanayoambatana na kansa ya damu au magonjwa yanayoathiri mfumo wa damu.
MATIBABU
Tiba sahihi ya tatizo hili ni
kutafuta chanzo cha tatizo la uume kusimama kwa muda mrefu
hadi mtu anapata maumivu. Endapo hali kama hii inatokea, basi
epuka kuvaa nguo za kubana au nguo za ndani, jifunge tu shuka
au msuli na endapo utavaa nguo kama suruali au bukta basi
hakikisha uume unauzungushia pamba ya kutosha, yaani usikwaruze
kwenye nguo ngumu na ikaleta kikwazo kitachoongeza maumivu.
Mgonjwa apelekwe haraka hospitali
ambapo atapatiwa matibabu. Wengi hutokewa na hali hii kwa
kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume bila ya
ushauri wa daktari.
UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME ‘IMPOTENCE’
Hali hii huitwa ukhanithi, hapa mtu
anashindwa kabisa kufanya tendo la ndoa kwa kutokuwa na uwezo, nguvu
zinapungua sana au zinakuwa zimekwisha kabisa.
Upungufu wa nguvu za kiume hutofautiana
na ugumba. Katika suala la ugumba mwanaume huwa hawezi kumpa mwanamke
mimba kwani mbegu zake za kiume huwa hazina ubora.
CHANZO CHA TATIZO
Tatizo hili limegawanyika katika
makundi au sehemu kuu mbili kitaalamu. Kwanza ni tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume la muda mfupi na pili ni tatizo la kudumu.
Aina hizi mbili huweza kumtokea
mwanaume yoyote lakini hili la muda mfupi humtokea mtu yeyote
kutokana na hali ya maisha ya kawaida kwani si kila siku mtu
anakuwa sawa. Majukumu ya kila siku yanaweza kukufanya ukapoteza
hamu na usiweze kuwa na nguvu za kutosha kwa wakati fulani.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment