ALIYEKUWA
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, leo anatarajiwa kuzungumza
na waandishi wa habari kueleza hatima yake ndani ya chama hicho.
Habari
zinasema amechukua hatua hiyo baada ya kuibuika wimbi la wana CUF
kumtaka arudi katika nafasi yake ya uenyekiti huku chama hicho
kikitangaza kufanyika kwa mkutano mkuu Agosti 21, mwaka huu.
Wakati
hayo yakiendelea taarifa za ndani zinaeleza kuwa mwishoni mwa wiki
iliyopita Profesa Lipumba, aliondoa barua yake ya kujiuzulu uenyekiti
na alikutana na Katibu Mkuu wa CUF na kujadili kwa kina suala hilo.
Chanzo
chatu cha uhakika ndani ya CUF kilisema baada ya mazungumzo ya kina,
Maalim Seif alimthibitishia Profesa Lipumba, kupokewa kwa barua yake
huku akimuomba asubiri ushauri wa wanasheria kuhusu hatima yake ya
kurejea ofisini.
“Kesho (leo) Profesa atazungumza na wana habari asubuhi na kikubwa ataeleza kwa kina hatima yake ndani ya CUF.
“Kikubwa tunategemea atafungua ukurasa mpya na kutangaza kukijenga chama chetu,” alisema mtoa habari wetu ambaye yupo karibu na Profesa Lipumba.
Profesa
Lipumba alijiuzulu nafasi hiyo Agosti 5, mwaka jana kwa kile
alichodai kutoridhishwa na hali ya mambo ikiwamo umoja ndani ya Ukawa na
kupokewa kwa aliyekuwa mgombea urais aliyekuwa anaungwa mkono na vyama
Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa.
Katika
siku za hivi karibuni kumekuwa na vuguvugu la wana CUF kuendesha
makongamano nchi nzima kutaka Profesa Lipumba arudi kwenye madaraka
kwa madai kwamba chama hicho kimekosa mtu imara upande wa Bara.
Licha
ya hali hiyo wanachama hao walikuwa wakitaka uitishwe Mkutano Mkuu
Maalumu ambao unatakiwa kujadili hoja ya kujiuzulu kwa Profesa Lipumba,
kwa mujibu wa Katiba ya CUF.
0 comments:
Post a Comment