Ripoti
ya Kampuni ya Lugumi kudaiwa kushindwa kutekeleza mradi wa utambuzi wa
vidole kwenye vituo vya polisi imerudishwa kwenye kamati ndogo
iliyoundwa kuchunguza sakata hilo baada kubaini mapungufu.
Akizungumza
katika viwanja vya Bunge, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za
Serikali, (PAC) Aeshi Hillaly alisema baada ya kukamilisha ripoti hiyo
itapelekwa katika kamati yake ili iweze kujadiliwa.
“Kamati
ndogo yenyewe iligundua kuwa kuna mapungufu kwenye hiyo ripoti, kwa
hiyo imeirejesha tena kwao ili kurekebisha mapungufu hayo kabla ya
kuileta kwenye kamati yangu tuijadili,” alisema.
PAC
iliunda kamati hiyo ndogo iliyokuwa inaongozwa na Japhet Hasunga
(Vwawa-CCM), ambayo imepewa kazi ya kuchunguza undani wa mkataba huo
wenye thamani ya Sh37 bilioni.
Aprili
23, mwaka huu, PAC ilikutana na kuteua wajumbe tisa watakaounda kamati
ndogo kuchunguza sakata hilo kwa undani, na kuandaa hadidu za rejea za
kufanyia kazi.
Baadhi
ya adidu za rejea zilizojadiliwa na PAC ni pamoja na kuangalia thamani
ya vifaa vilivyonunuliwa na hali halisi ya soko na kama kulikuwa na
ulazima wa kutoa kazi hiyo kwa mbia mmoja.
Kampuni hiyo ilitakiwa kufunga mashine 108 katika vituo vya polisi lakini ilifunga 14 tu.
0 comments:
Post a Comment