IMEVUJA! Safari za mara kwa mara mkoani Morogoro, zinazofanywa na staa
wa filamu za Kibongo, Wastara Juma zinadaiwa kuchangizwa baada ya
kumnasa kigogo mmoja mkoani humo.
“Yaani siku hizi Wastara hatulii Dar ilipo familia yake, amekuwa akisafiri Morogoro kila kukicha, yaani hivi sasa ni mapenzi motomoto, lakini ni kwa siri sana hataki ijulikane,” kilisema chanzo chetu hicho.
Baada ya kuunyaka ‘ubuyu’ huo, paparazi wetu alimtafuta Wastara na alipopatikana, alikana taarifa hizo na kudai safari zake za mara kwa mara mkoani humo ni kwa vile huko ni nyumbani kwao.
“Hizo habari siyo kweli, watu wanapenda tu kuongea, Morogoro huwa naenda kwa sababu ya mambo mawili, kwanza kule ndiko nilikozaliwa hivyo huwa naenda kuwaona ndugu zangu na pili huwa naenda kwa sababu nina kituo cha kulelea watoto yatima, kwa hiyo huwa naenda kuwaangalia,” alisema Wastara.
Chanzo:GPL
0 comments:
Post a Comment