Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>>Maneno ya Zitto Kabwe Baada ya Msiba wa Mzee Aboud Jumbe "Nchi Hii Wakubwa Wakigombana Huwa Hawasameheani?...Fahamu zaidi hapa.
Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, Makamu wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
ametangulia mbele ya Haki. Inna lillah waina ilaih raajiun.
Mzee Jumbe atakumbukwa katika historia ya Tanzania Kama Kiongozi
aliyeamini na kusimamia anachoamini bila kujali madhara yake. Alipoteza
nafasi zake za Uongozi Kwa sababu ya msimamo wake kuhusu muundo wa
Muungano kutoka Serikali 2 kwenda Serikali 3.
Mzee Jumbe ameacha maandiko kupitia kitabu chake cha The Partnership
ambacho ndugu yetu Ali Ally Saleh ' Alberto ' alipata heshima ya
kukifasiri.
Pia Mzee Jumbe ameacha ' memoir ' yake ambayo ninaamini walioachiwa sasa
wataweza kuitoa ili dunia ipate kujua mengi ambayo labda hatujui kuhusu
Nchi yetu.
Hivi hapa Tanzania kuna Hata barabara yenye jina la Aboud Jumbe Mwinyi? Daraja? Nchi hii wakubwa wakigombana huwa hawasameheani?
Wazanzibari wanaweza kutumia msiba wa Mzee Jumbe kujenga maridhiano na kuanza kujenga Zanzibar kwa pamoja?
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>Wanafunzi 316 Waliofukuzwa Chuo Kikuu cha St. Joseph Wafungua Kesi Mahakamani.Fahamu zaidi hapa.
MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa kibali cha kufungua kesi ya
uwakilishi, kwa wanafunzi wanne, waliofukuzwa katika Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Joseph kwa madai ya kutokuwa na sifa za kudahiliwa kwenye vyuo
vikuu… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Wapinzani Wataka Wabunge wa CCM Wasioongea Bungeni Nao Wanyimwe Posho.Fahamu zaidi hapa.
KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imelitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwafutia posho wabunge wa CCM
wanaofika kwenye vikao vya Bunge hilo na kukaa kimya bila kuchangia
jambo lolote hata kwa maandish… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Serikali Yatangaza Vita Dhidi ya Majambazi na Watu Wanaojihusisha na Mauaji.Fahamu zaidi hapa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni ametangaza vita dhidi ya majambazi na watu wanaojihusha na mauaji.
Alisema
Serikali imelazimika kutangaza vita hivyo baada ya kutokea matukio 41
yaliyohusi… Read More
#YALIYOJIRI>>>Maalim Seif ziarani Marekani.Anatarajiwa Kuieleza Jumuiya ya Kimataifa Kilichojiri Kwenye Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.Fahamu zaidi hapa.
Katibu
Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amekwenda Marekani na kesho
ataiambia jumuiya ya kimataifa, kilichojiri kwenye Uchaguzi Mkuu na
kusababisha chama chake kususia uchaguzi wa marudio wa Rais wa Zanzibar
ulioi… Read More
#YALIYOJIRI>>>>OLE MEDEYE ATIMKA CHADEMA,AHAMIA UDP LEO.Fahamu zaidi hapa.
Kada wa Chadema na mbunge wa
zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye ametangaza leo rasmi
kuhamia chama cha UDP.Ole Medeye amezungumza hayo mbele ya mkutano wa
waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za M… Read More
0 comments:
Post a Comment