Monday 23 May 2016

Busu la Penny Lazua Utata.Fahamu zaidi hapa.

Busu ambalo mtangazaji Peniel Mungilwa ‘Penny’ amempiga mwigizaji Shamsa Ford limezua utata kufuatia watu kumhusisha na tabia isiyofaa.
ayo yalijiri hivi karibuni baada ya mtangazaji huyo kutupia picha kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram ndipo wafuasi wa mtandao huo walipoanza kumsema vibaya wakidai anajiabisha kwa vitendo visivyofaa. 

Alipoulizwa kuhusiana na jambo hilo, Penny alisema: “Hayo ni maneno tu huwa hayani sumbui, lile ni busu la kawaida. Nimembusu kama rafiki lakini nawashangaa hao wanaozua mambo yao na kuzungumza tofauti.”
Chanzo:GPL

0 comments:

Post a Comment