Saturday 28 May 2016

#MICHEZO>>>>WAPINZANI WA YANGA CAF WAANZA KUTOA SABABU.Fahamu zaidi hapa.

TIMU ya soka ya Medeama ya Ghana, imesema itakuwa shughuli pevu kukutana Yanga SC ya Tanzania katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, kwa sababu sasa inafundishwa na kocha wao wa zamani, Mholanzi Hans van der Pluijm.

Mtendaji Mkuu wa Medeama, James Essilfie amesema hayo baada ya kupangwa droo ya makundi ya Kombe la Shirikisho, wao wakiangukia Kundi A pamoja na Yanga, TP Mazembe ya DRC na Mo Bejaia ya Algeria.

“Yanga inafundishwa na Hans Van der Pluijm, kocha wa zamani wa Medeama na kucheza nao itakuwa mechi nzuri,” alisema na kuongeza; “Tumefurahishwa na makundi, timu nyingine katika kundi zitasaidia kuonesha ubora wa Medeama.

Wengi walitilia shaka uwezo wetu tulipopangiwa Mamelodi Sundowns (ya Afrika Kusini) katika hatua ya mchujo, lakini tumethibitisha ubora wetu,” amesema Essilfie ambaye timu yake iliitoa Mamelodi na kuingia kwenye makundi.

0 comments:

Post a Comment