Monday 23 May 2016

Harmonize Afungukia Penzi la Wolper.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya tetesi kuvuma kuwa ukaribu wa kimapenzi kati ya muigizaji Jackine Wolper na staa wa Bongo Fleva Harmonize ni wa kuigiza na kutafuta kiki, Harmonize ameamua kufunguka juu ya mahusiano hayo.
Akizungumza na eNewz Harmonize alisema kuwa muda ukifika atampelekwa mchumba wake huyo kwao kwa ajili ya kumtambulisha kwa wazazi wake huku wakiwa na ndoto za kujenga familia pamoja.

Pia Harmonize aliiambia eNewz kuwa alikutana na Wolper akiwa hana mchumba wala hakuwa na pete ya uchumba kwa hiyo yeye mambo ya pete hayafahamu, huku ikiwa inafahamika kuwa mpenzi wake huyo tayari alishakuwa na mchumba ambae alikuwa amemvika pete ya uchumba.
eatv.tv

0 comments:

Post a Comment