Friday 27 May 2016

Iyobo Ametusitiri kwa Aunt-Steve Nyerere.Fahamu zaidi hapa.

Staa wa filamu na vichekesho Bongo, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’, amewavunja mbavu watu baada ya kusema kuwa anamshukuru sana Moses Iyobo kwa kukubali kuzaa na Aunt Ezekiel, kwani kwa kufanya hivyo amewasitiri wasanii wote wa Bongo Muvi.
Akizungumza wakati alipoalikwa kwenye bethidei ya mtoto wa mastaa hao iliyofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Serena jijini Dar, Steve alisema kuwa kitendo alichofanya Iyobo ni cha kishujaa sana kwani mpaka kumzalisha Aunt haikuwa kazi rahisi.

“Unajua watu wengi walishindwa lakini Iyobo ni kidume kabisa, tena katusitiria dada yetu na hatimaye sasa hivi ana mtoto. Ninachomsihi ni kuongeza mwingine fasta,” alisema Steve.
Chanzo: GPL

0 comments:

Post a Comment