Thursday 26 May 2016

#MICHEZO>>> WAMBURA AULA KWA CAF.Fahamu zaidi hapa.

 Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Michael Richard Wambura kuwa Kamishina wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na Msumbiji unaotarajiwa kufanyika jijini Kigali, Juni 3, 2016. Wambura ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), atakuwa Balozi mzuri katika mchezo huo unaokutanisha timu ambazo nchi imepana nazo. Msumbiji iko Kusini mwa Tanzania wakati Rwanda iko Magharibi mwa Tanzania.

0 comments:

Post a Comment