Saturday 28 May 2016

#YALIYOJIRI>>>MAKONDA AWAPONDA WANAOIGA ‘UZUNGU’.Fahamu zaidi hapa.

 WATANZANIA wametakiwa kuwa wazalendo na kuacha kutumia tamaduni za nje, ambazo zinachangia mmomonyoko wa maadili.

Hayo yalisemwa  na Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda alipotembelewa ofisini kwake na wanafunzi wanaosoma shule za Feza kutoka nchi 15 waliokuja nchini kutangaza utamaduni wao.

Alisema Watanzania wengi wamekuwa wakiiga tamaduni za kigeni na kusahau utamaduni wao, ambao ungeweza kuwatambulisha katika nchi nyingi na kuijenga sifa ya nchi.

Aliongeza kuwa ni jambo la kushangaza, kuona watu kutoka nchi mbalimbali wakija Tanzania kutangaza utamaduni wao ; na Watanzania wakikaa na kuishia kuiga tamaduni za watu na kuacha tamaduni zao kupotea.

“Utamaduni mkubwa ambao tunaweza kuutangaza ni lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo pekee, inaweza kuitangaza nchi yetu duniani kote na ikajenga heshima ya nchi kuliko kufuata tamaduni ambazo haziwajengi Watanzania zaidi ya kuwaharibu,” alisema Makonda.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Feza Tanzania, Kadik Dakicek, ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, wakishirikiana na International Festival Language and Culture, alisema madhumuni makubwa ya ujio wa wanafunzi hao ni kutangaza tamaduni zao na Tanzania ndio mwenyeji wa shughuli hiyo kwa mwaka huu.

“Tumewahi kufanya tamasha kama hizi za kutangaza utamaduni katika nchi mbalimbali na mwaka huu tunafuraha kuona Tanzania inakuwa mwenyeji wa tamasha hili, tunaamini kupitia tamasha hili, nchi itajifunza mambo mbambali ambayo yatawasaidia kutangaza utamaduni,” alisema Dakicek.

0 comments:

Post a Comment