Saturday 28 May 2016

#YALIYOJIRI>>>>WAZIRI MKUU MAJALIA ABAINI CHANGAMOTO ZA MABASI YA MWENDOKASI.Fahamu zaidi k hapa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua utendaji kazi kwenye Mabasi ya Mwendokasi yanayotoa huduma katika Jiji la Dar es Salaam na kubaini changamoto kadhaa ambazo amesema zitarekebishwa kadri mradi unavyoendelea.

Waziri Mkuu ambaye alilipa nauli na kupanda basi namba 23 lenye usajili namba T125 DGW kuanzia Kituo cha Ferry, Kivukoni, ametumia muda wa dakika 50 kufika Kimara mwisho kwa kutumia usafiri huo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari akiwa Kimara mwisho mara baada ya kumaliza ziara hiyo fupi Waziri Mkuu alisema aliamua kufanya ziara hiyo.

0 comments:

Post a Comment