Wednesday 25 May 2016

#MICHEZO>>>>YANGA KWA MARA NYINGINE TENA YAENDELEZA UBORA KWA KUCHUKUA KOMBE LA "FA".FAHAMU ZAIDI HAPA.

 Yanga imefanikiwa kutwaa ndoo zote msimu huu zinazosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) baada ya kuichapa Azam FC kwa bao 3-1 kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA (Azam Sports Federation Cup) mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa taifa.
 Shukrani za pekee zinaenda kwa mshambuliaji wa Burundi Amis Tambwe kwa magoli yake mawili yaliyoisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
 Tambwe aliiandikia Yanga bao la kwanza dakika za mwanzo kipindi cha kwanza ambalo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
 Dakika ya 47 kipindi cha pili, Tambwe aliifungia Yanga bao la pili lakini dakika moja baadaye Didier Kavumbagu aliirejesha Azam kwenye mchezo baada ya kuifungia bao ambalo ndiyo lilikuwa la kufutia machozi.
 Wakati Azam wakipambana kusawazisha goli, Deus Kaseke alizima ndoto za Azam baada ya kufunga bao la tatu na kuihakikishia Yanga ubingwa wa FA.
 Ubingwa huo unakuwa ni wa tatu kwa Yanga kwa mashindano ya ndani ambayo yanasimamiwa na TFF, Yanga ilianza kwa kutwaa Ngao ya Jamii mapema kwezi August mwaka jana kwa kuifunga Azam, kisha wakatwaa taji la VPL kabla ya kumaliza na FA Cup.
 Ubingwa wa FA Cup unaipa Yanga kiasi cha shilingi milioni 50 za kitanzania ambazo zimetolewa na mdhamini wa mashindano hayo ambaye ni Azam Media.
Je wajua?

  • Yanga na Azam zimekutana leo kwa mara ya tano kwenye mechi tofauti ndani ya msimu huu, mchezo wa kwanza ulikuwa wa ngao ya jamii Yanga ikashinda kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka suluhu (0-0). Klabu hizi zikakutana kwa mara nyingine kwenye ligi mzunguko wa kwanza October 17, 2015 na kwenda sare ya kufungana bao 1-1. Mara ya tatu zikakutana kwenye mchezo wa Mapinduzi Cup hatua ya makundi na kulazimishana sare ya goli 1-1 kabla kukutana kwenye mchezo wa ligi raundi ya pili March 5, 2016 na kutoka sare kwa mara nyingine tena ya kufungana goli 2-2.
  • Azam wamemaliza katika nafasi ya pili katika kila mashindano ya ndani waliyoshiriki msimu huu huku Yanga wakimaliza katika nafasi ya kwanza, Azam ilipoteza Ngao ya Jamii na kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Yanga, ikashindwa kutwaa taji la VPL ambalo lilinyakuliwa na Yanga na wao wakamaliza nafasi ya pili kisha wamekuwa washindi wa pili kwenye michuano hii ya FA Cup.
  • Katika mechi tano za mwisho ambazo Yanga na Azam zimekutana, yamefungwa jumla ya magoli 12; August 22, 2015: Ngao ya Jamii Azam 0-0, October 17, 2015: VPL Yanga 1-1 Azam, January 5, 2016 Azam 1-1 Yanga, March 5, 2016: VPL Azam 2-2 Yanga na May 25, 2016 Yanga 3-1 Azam.
  • Yanga ilianzisha wachezaji wake watano wa kimataifa (Vicent Bosou, Haruna Niyonzima, Thaban Kamusoko, Amis Tambwe na Donald Ngoma) wakati Azam Jean Mugiraneza ni mchezaji pekee aliyeanza kwenye kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation Cup.
Kikosi cha Azam FC: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Aggrey Morris, Abdallah Kheri, Jean Mugiraneza, Ramadhani Singano, Mudathir Yahya, Himid Mao na Farid Musa.
Walioanzia benchi: Mwadini Ali, Said Murad, Shabani Idd, Didier Kavumbagu, Ame Ali, Michael Balou na Frank Domayo.
Kikosi cha Yanga: Deogratius Munishi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Vicent Bosou, Simon Msuva, Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Amis Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke.
Walionzania benchi: Ally Musatafa, Mbuyu Twite, Nadir Haroub Cannavaro, Salum Telela, Geofrey Mwashiuya, Haji Mwinyi, Matheo Anthon.

0 comments:

Post a Comment