Home »
Michezo
» #BREAKING NEWS>>>>KOCHA WA ZAMANI WA NIGERIA STEVEN KESHI AFARIKI DUNIA.Fahamu zaidi hapa.
Nigeria wamepata pigo baada ya taarifa kwamba Stephen Okechukwu Keshi aka ‘the Boss’ amefariki ghafla mapema leo asubuhi.
Mchezaji huyo wa zamani ambaye pia alimpoteza mkewe Kate mwaka jana
aliyekuwa na umri wa miaka 33, kwa ugonjwa wa kansa, inaarifiwa amekufa
kutokana na matatizo ya moyo huko Benin, Edo State.
Kwa mujibu wa wanafamilia na marafiki zake wa karibu, Keshi
hakuonesha dalili zozote za kuumwa. Alikuwa akiishi na watoto wake wanne
pamoja na mama yake mzazi.
Mwaka 2013 aliweka rekodi baada ya kuipa Nigeria kombe la Mataifa ya
Afrika na kuwa kocha pekee mzawa kufanya hivyo. Pia anashilikilia rekodi
ya kuwa kocha wa pili kushinda kombe hilo akiwa kama mchezaji na
baadaye kocha.
Mtu mwingine aliyeweza kufanya hivyo ni Mahmoud El-Gohary wa Misri.
Aliiwakilisha Nigeria kuanzia mwaka 1982, akiwa na umri wa miaka 20,
mpaka mwaka 1994, mara nyingi aliitumikia Nigeria kama nahodha na
kufunga magoli muhimu hasa ukizingatia nafasi yake aliyokuwa akicheza,
kama beki wa kati.
Vile vile aliwahi kuifundisha Togo na Nigeria katika kombe la dunia, vilevile Mali.
Related Posts:
#MICHEZO>>>>>BALOTELLI BANA! KAIFUNGIA TIMU YAKE BAO LA USHINDI, NDANI YA DAKIKA 4 AKALA NJANO MBILI, IKAWA RED.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Ukitaka mwanao apate shida, mwite Balotelli, maana hili jina, mwenyewe Mario Balotelli ni shida tupu.
Jana
ameonyesha kweli ana uwezo wa kucheza soka, kafunga bonge la bao na
kuisaidie Nice kushinda kwa mabao 2-… Read More
#MICHEZO>>>>Jamhuri Kiwelu Julio Ametangaza Rasmi Kuachana na Kazi ya Ukocha.Fahamu zaidi hapa.
Kocha wa klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu Julio, October 2
2016 ametangaza kujiuzulu kufundisha soka la nchini Tanzania kufuatia
kutoridhishwa na maamuzi yanayofanywa na marefa uamuzi huo umeonekana
kuwasht… Read More
#MICHEZO>>>YANGA YAOMBA IUTUMIE UWANJA WA AMAAN ZANZIBAR KWA LIGI KUU BARA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Uongozi
wa klabu ya Yanga, umeandika barua kuomba kuutumia Uwanja wa Amaan
mjini Zanzibar kwa ajili ya mechi zake za Ligi Kuu Bara na mashindano
mengine.
Yanga
imechukua uamuzi huo baada ya Serikali kutangaza kuif… Read More
#MICHEZO>>>>> HATIMAYE GUARDIOLA AKARIBISHWA ENGLAND MAN CITY IKIBUTULIWA MABAO 2-0 NA TOTTENHAM.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Man
City imeanza kuonja uchungu wa kipigo baada ya kupoteza mechi yake ya
kwanza ya Ligi Kuu England kwa kupigwa mabao 2-0 na Tottenham.
Man
City inayonlewa na Kocha Pep Guardiola, ilionyesha soka safi lakini
ikas… Read More
#MICHEZO>>>>Rigobert Song afikishwa hospitali kwa matatizo ya ubongo.Fahamu zaidi hapa.
Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon na kocha wa
sasa wa timu ya taifa ya vijana wadogo ya Cameroon, Rigobert Song
amefikishwa mjini Yaounde, Cameroon baada ya kuugua ghafla.
Taarifa kutoka vyanzo vya ha… Read More
0 comments:
Post a Comment