Siku
chache baada ya Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya
mikutano nchi nzima kwa lengo la kuishtaki kwa wananchi Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, CCM wamejibu mapigo
kwa kuapa kuwafuata kila kona watakayopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa CCM,
Christopher Ole Sendeka alisema kuwa chama hicho hakiwezi kuvumilia
kuona Chadema wanazunguka kuharibu taswira ya Rais Magufuli na Serikali
yake ambayo alieleza kuwa imefanya kazi kubwa kuwatumikia wananchi
katika kipindi kifupi.
Alisema
kuwa wamepata taarifa zisizo na shaka kuwa Kamati Kuu ya Chadema
iliyokutana Mei 16 mwaka huu ilibaini kuwa kwa muda mfupi, Magufuli
ametekeleza ajenda zote ilizokuwa ikinadi wakati wa Uchaaguzi Mkuu.
Ole
Sendeka alisema kuwa utendaji wa Rais Magufuli unatuma ujumbe wa
dhahiri kuwa Chadema watashindwa tena katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Aliongeza kuwa malalamiko ya udikteta wanayoyasambaza yanaonesha kuwa hawana mjadala wowote wa kumkosoa Rais Magufuli.
“Tunawaonya
viongozi wa Chadema. Wanapaswa kutumia majukwaa hayo kunadi sera za
Chadema. Nataka kuwahakikishia kuwa, kama Chadema wataenda sehemu fulani
Jumatatu, sisi tutakuwa pale Jumanne kusafisha hali ya hewa kwa
kuwaeleza ukweli wananchi,” alisema Ole Sendeka.
Chadema
wamepanga kufanya mikutano nchi nzima kwa kile walichoeleza kuwa ni
kuishtaki Serikali kwa wananchi kuhusu mwenendo wa Serikali ikiwa ni
pamoja na kubanwa kwa Demokrasia na Bunge kwa ujumla na utumbuaji majipu
usiofuata sheria na taratibu.
0 comments:
Post a Comment