TAARIFA YA JESHI LA POLISI
Ndugu zangu waandishi wa habari,
Katika
siku za hivi karibuni, Jeshi la Polisi nchini, limepokea taarifa kutoka
kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya mikutano na maandamano .
hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake vya mbalimbali vya
habari limebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi
kutotii sheria za nchi (Civil disorder).
Aidha vyama vingine vya siasa vimeonyesha dhamira ya kupinga kile ambacho kitasemwa na wapinzani wao.
Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya kisiasa.
Kwa
hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapiga marufuku maandamano na
mikutano ya hadhara kuanzia tarehe 07/06/2016 hadi hapo hali ya usalama
itakapotengemaa.
Jeshi la Polisi linawataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi.
Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili.
Aidha
Jeshi la Polisi linawataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye
lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi
waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii.
Asanteni sana kwa kunisikiliza .
Imetolewa na:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi.
0 comments:
Post a Comment