Wednesday, 8 June 2016

#YALIYOJIRI>>>ZITTO: SERIKALI YA MAGUFULI INAJENGA UOGA WA WATU KUSEMA UKWELI.Fahamu zaidi hapa.

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli licha ya kasi yake ya kubana matumizi na kuziba mianya ya rushwa kwa maendeleo ya Taifa, imetajwa kuwa serikali inayokandamiza Demokrasia kwa kuzuia Uhuru wa Kutoa maoni.

Na hii inatokana na matamko mbalimbali ikiwemo ya Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama vya siasa, kubadilisha mfumo wa urushaji wa  matangazo ya Bunge moja kwa moja (Live), kuwa simamisha baadhi ya wabunge waliokuwa wakidai urushwaji wa Bunge Live vimetajwa kama vielelezo vya kukandamiza uhuru wa mawazo na kuikandamiza Demokrasia.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe alipoitwa kuhojiwa kuhusu maudhui ya hotuba yake aliyoitoa June 5 alipokuwa anazungumza na wakazi wa Mbagala kuhusu suala ukandamizwaji wa Demokrasia unaooneshwa kwa vitendo na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli.


0 comments:

Post a Comment