Saturday 29 August 2015

#MICHEZO>>>Arsenal wang'aaa huku Chelsea wateleza ligi kuu England.Fahamu zaidi hapa.

Ligi kuu ya England imeendelea leo na kushuhudia vigogo Chelsea na Liverpool wakiangukia pua kwa kuchezea kichapo kwa mitindo tofauti.
Chelsea imefungwa na Crystal Palace mabao 2-1, katika dimba la Stamford Bridge mabao crystal Palace yakifungwa na Bakary Sako dakika ya 65 na Joel Ward dakika ya 81 huku bao la kufutia machozi likifungwa na Radamel Falcao dakika ya 79.
Liverpool imechapwa na West Ham United mabao 3-0 ikiwa Anfield, kwa mabao ya Manuel Lanzini 3, Mark Noble 29 na Diafra Sakho dakika ya 90.
Mechi hiyo pia imeshuhudia Philippe Coutinho wa Liverpool akitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 53 na Mark Noble naye akilambwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 79.
Manchester City na Arsenal zimeondoka na ushindi ambapo sasa Man City imezidi kujikita kileleni kwa kushinda michezo minne mfululizo hadi sasa.

0 comments:

Post a Comment