Saturday 22 August 2015

#YALIYOJIRI>>>>Wasichana walio katika mazingira magumu wahitimu Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.



Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto  Mhe. Dkt. Pindi H. Chana (Mb)akimpongeza Bi. Jane Malyi kiongozi wa wahitimu wa mafunzo ya ujasiriamali na urembo mara baada ya kutoa neno fupi kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo katika chuo Kikuu Huria cha Tanzania, jijini Dar es salaam
Na erasto Ching’oro  Wasichana 22 kutoka mazingira hatarishi wamehitimu mafunzo ya ujasiriamali, mawasiliano, ususi wa nywele na urembo katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania jijini Dar es salaam na kutunukiwa vyeti vya umahiri na Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Mhe. Dkt. Pindi H. Chana ambaye alikuwa mgeni rasimi kwenye mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo (OUT) tarehe 20 Agosti, 2015. 
Mapema mwezi Januri, 2015 Chuo Kikuu Huria kwa ushirikiano na asasi ya ‘Nafasi Opportunity Society (NOS)’ ya nchini Canada walibaini wasichana 22 wanaoishi katika mazingira hatarishi kutoka mikoa mbalimbali na kuwapa fursa ya kujiunga na mafunzo ya ujasiriamali, ususi na ulembo kwa lengo la kuwawezesha kupata stadi na weledi ili kuboresha kazi zao.  Katika kufanikisha lengo hilo asasi ya NOS ilikubali kugharimia mafunzo ya wasichana hao kuanzia Januri 2015 hadi Agosti, 2015 na wote kuweza kuhitimu na kutunukiwa vyeti na Mhe. Pindi Chana. Mgeni Rasimi Mhe. Pindi aliwapongeza waliohitimu maana mafunzo waliyopata yamewaongezea mbinu katika ajira. 
Pili, wameweza kupata maarifa na stadi za ujasiriamali hivyo kuwawezesha kujiajiri na kuajiri wengine. Fursa ya mafunzo waliyopata wasichana itaongeza thamani ya utumishi wao katika soko la ajira maana wamepata mafunzo kutoka katika Chuo makini (OUT) na huduma ya wahitimu hao itawawezesha kupata kazi zenye staha katika soko na watatangazia vizuri nafasi ya Chuo Kikuu Huria Tanzania katika kumwendeleza mwanamke. Mhe. Pinda alisisitiza kuwa elimu ya urembo ni fani ambayo inahitajika kwa wanaume na wanawake wa vijijini na mijini. Kama fani hii ya urembo itaendelezwa itaongeza nafasi za ajira kwa wasichana na wavulana kwa kiasi kikubwa maana mahitaji yake ni ya hakika katika soko. 
Awali Kaimu Mkuu wa Chuo Huria cha Tanzania Prof. matern Victor, alieleza kuwa mafunzo hayo maalum kwa wasichana wanaoishi katika mazingira magumu yalilenga kujenga uwezo wa familia na jamii katika mikoa na kwamba kama rasilimali fedha ikipatikana na jamii ikaendeleza juhudi za kutoa haki sawa ya elimu kwa wote wasichana wengi wenaweza kufikiwa kupitia Ofisi za mikoa. 
  Toa maoni yako hapa.

0 comments:

Post a Comment