Sunday 23 August 2015

#YALIYOJIRI>>>Miezi 6 jela kwa wapenzi wa jinsia moja huko senegal. Fahamu hapa.



Watu 7 wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kuenda kinyume na madili.
Watu hao walipatikana na hatia katika mahakama moja ya Senegal kwa kushiriki ngono na watu wa jinsia yao.
Mahakama mjini Dakar ilielezwa kuwa wanaume hao walinaswa katika mtego uliowekwa na maafisa wa Polisi katika makazi ya mmoja wao.
Mama mzazi wa mmoja wa watuhumiwa alikiri kuwa mwanawe alikuwa na mpenzi wa jinsia yake japo alikataa kufika mahakamani kutoa ushahidi.
Ngono ya wapenzi wa jinsia moja ni haramu nchini Senegal.

0 comments:

Post a Comment