Sunday 27 September 2015

#MICHEZO>>>Azam yaendeleza ushindi baada kuifunga Mbeya City.Fahamu zaidi hapa.

Azam FC yaendeleza wimbi la ushindi  katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa mabao 2-1 Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mchezo huu ulioharibiwa na maamuzi ya hovyo ya Martin Saanya wa Morogoro, aliyesaidiwa na Julius Kasitu wa Shinyanga na Sylvester Mwanga wa Kilimanjaro, hadi mapumziko Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Kiungo Mudathir Yahya Abbas aliifungia Azam FC bao katika dakika ya 10 baada ya kuuwahi mpira uliookolewa kufuatia yeye mwenyewe kupiga shuti na lililookolewa kabla wa kuuwahi mpira na kufunga.
Timu zote zilishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza na Mbeya City walipoteza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 44 baada ya shuti la Joseph Mahundi kugonga mwamba na kurudi uwanjani na kumkuta Serge Wawa Pascal aliyeokoa.
Kipindi cha pili, mchezo uliendelea kuwa wa staili ile ile, timu zote kushambuliana kwa zamu.


Mshambuliaji Kipre Herman Tchetche kutoka Ivory Coast aliifungia Azam FC bao la pili dakika ya 52 akimalizia pasi ya Sure Boy.
Mbeya City walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Raphael Alpha dakika ya 56.
 
Kipre Tchetche aliifungia Azam FC bao ambalo lingekuwa la tatu, lakini refa Saanya akasema mfungaji aliotea.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 12, sawa na Mtibwa Sugar na Yanga SC, zikifuatiwa na Simba SC yenye pointi tisa.

Kikosi  cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, David Mwantika, Racine Diouf, Serge Wawa Pascal, Jean Baptiste Mugiraneza, Mudathir Yahya/Himid Mao dk46, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco, Kipre Tchetche/Alan Wanga dk78 na Farid Mussa. 
Mbeya City; Hannington Kalyesebula, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Juma Nyosso, Christian Sembuli, Steven Mazanda, Richard Peter, Raphael Alpha, George Mlawa/David Kambole dk85, Themi Felix/Meshack Samuel dk58 na Joseph Mahundi. 

0 comments:

Post a Comment