Monday 21 September 2015

#MICHEZO>>Hamis Kizza aibeba Simba.Fahamu zaidi hapa.

Timu ya Simba SC ikicheza mechi yake ya tatu ya ligi katika uwanja wake wa nyumbani imeifunga timu ya Kagera Sugar  kwa magoli 3 – 1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Magoli yote ya Simba yalifungwa na mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda Hamis Kizza “Diego” katika kipindi cha kwanza na cha pili cha mchezo wa leo. Kizza alifunga goli la kwanza katika dakika ya 31 kipindi cha kwanza baada ya kazi nzuri kutoka kwa mchezaji Awadhi Juma na baadae kufunga magoli mengine mawili katika dakika ya 46 na 92 katika kipindi cha pili cha mchezo.

Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya mechi kocha mkuu wa Simba Dylan Kerr alisema “nimefurahishwa sana na kikosi changu kwa mchezo safi wa leo, wamecheza kwa kujituma na kuweza kupata ushindi mzuri. Sasa tunaweka nguvu zetu kwa mechi yetu inayofuata tarahe 26, September 2015”.

0 comments:

Post a Comment