Sunday 13 September 2015

#YALIYOJIRI>>>Rais Jakaya Kikwete akiwa anafungua Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Arusha.Fahamu zaidi hapa.

  Mkuu wa Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu Meja Jenerali Ezekiel Kyunga kulia akimuonyesha Amiri Jeshi Mkuu Rais Mh.Jakaya Mrisho Kikwete maeneo mbalimbali ya Chuo hicho muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua Chuo hicho eneo la Duluti nje kidogo ya mji wa Arusha leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Mh.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vitabu katika maktaba ya Chuo cha Unadhimu na Ukamanda alichokizindua leo.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Mh.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia mitaala inayofundishwa katika chuo cha Ukamanda na Unadhimu katika moja ya kompyuta chuoni hapo muda mfupi baada ya kuzindua chuo hicho eneo la Duluthi nje kidogo ya mji wa Arsuha leo.Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Ezekiel Kyunga.
  Rais Mh.Jakaya Mrisho kikwete akitoa ushauri wakati akikagua majengo ya Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo eneo la Duluti nje kidogo ya mji wa Arusha leo. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda,kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange, Wapili kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Meja Jenerali Ezekiel Kyunga na kulia ni mwakilishi kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu Balozi Ibrahim Al Suweidy.umoja wa Falme za Kiarabu ulishirikiana na Serikali kufadhili ujenzi wa Chuo hicho.
 Rais Mh.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Chuo cha Ukamanda na unadhimu Dukuti nje kidogo ya mji wa Arusha.
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Chuo cha Unadhimu na ukamanda huko Arusha.

0 comments:

Post a Comment