Saturday 26 September 2015

#MICHEZO>>>Yanga FC yaonesha Ubora wao mbere ya watani wao Simba FC hiyo jana.Fahamu zaidi hapa.

Timu ya Yanga FC Baada ya kukosa ushindi kwa kipindi cha miaka kadhaa hatimaye leo  wamewafunga watani zao wa  Simba FC kwa ushindi wa goli 2-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara wa raundi ya nne ulipigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Amis Tambwe na Malimi Busungu wameibuka mashujaa kwenye mchezo wa leo lakini sifa pekee zinaenda kwa Busungu aliyeingia kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Msuva na kutengeneza bao lililofungwa na Tambwe dakika ya 44 kipindi cha kwanza kabla ya yeye kufunga bao la pili dakika ya 79 kipindi cha pili.
Simba FC watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kufunga mabao kipindi cha kwanza wakati wanatawala mchezo kabla ya mambo hayajawa magumu baadae walipofungwa.

Mpira ulianza kwa kasi huku Simba wakitawala sana sehemu kubwa ya mchezo na mara nyingi walitengeneza mashambulizi lakini safu ya ushambuliaji iliyokuwa inaongozwa na Hamis Kiiza pamoja Mussa Mgosi ilishindwa kutumia nafasi hizo kufunga magoli.

Muda mwingi wa kipindi cha kwanza Yanga walikuwa wakishambuliwa huku Simba wakitengeneza mashambulizi yao kupitia upande wa winga ya kulia na kumpa Haji Mwinyi kazi ya ziada.
Baada ya kuonekana mchezo umemkataa Simon Msuva, kocha wa Yanga alifanya mabadiliko ndani ya kipindi cha kwanza kwa kumtoa Msuva na nafasi yake ikachukuliwa na Malimi Busungu ambaye alionesha uhai mkubwa na badae kutoa pasi ya goli lililofungwa na Amis Tambwe.

Kipindi cha pili mambo yaligeuka baada ya Yanga kumiliki mchezo na kufanya mashabulizi kadhaa kwenye lango la Simba yaliyokuwa na madhara.

0 comments:

Post a Comment