Monday 21 September 2015

#YALIYOJIRI>>>Lukuvi agoma kutamka kuzindua Halmashauri maana viongozi ndiyo watendaji.Fahamu zaidi hapa.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameacha hali ya kutokufahamika kwenye Wizara hiyo baada ya kusita kutamka maneno ya kuzindua Halmashauri ya 11 ya wapima ardhi katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Wizara hiyo.

Hatua ya Waziri kutotamka uzinduzi rasmi umetokana na kushuhudia viongozi wa Halmashauri hiyo yenye jukumu la kusajili Wapima Ardhi na Wathamini katika kusimamia taaluma na mwenendo wa utendaji katika masuala ya kupima ardhi, ndiyo watendaji wakuu wa Wizara.

Akizungumzia mkanganyiko huo, Waziri Lukuvi amesema haiwezekani yakawepo mazingira ya kutenda haki ikiwa viongozi wenye jukumu la kusimamia Halmashauri hiyo ili iweze kusimamia na kuondoa migogoro katika sekta ya ardhi ndio, hao hao watendaji wakuu katika Wizara hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Waziri amependekeza sheria ya kuanzisha halmashauri hiyo ibadilishwe ili kuwaondoa watendaji hao ambao miongoni mwao wanatuhuma za kuhusika na migogoro ya ardhi ili chombo hicho kiongozwe na watu kutoka nje ya serikali.

Wajumbe wapya wa Halmashauri hiyo wanaongozwa na Justo Lyamuya kama Mwenyekiti na Katibu ni Nassor Duduma, wote ni watendaji katika Wizara hiyo.
Chanzo
                           http://www.wavuti.com/2015/09/lukuvi-agoma-kutamka-kuzindua.html

0 comments:

Post a Comment