Thursday 22 October 2015

#Breaking News>>>Nape Nnauye Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama cha (CCM) anusurika kifo katika ajali iliyotokea leo eneo la Kilwa.Fahamu zaidi hapa.

Nape Nnauye ambae ni Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama cha (CCM), amepata ajali mbaya akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.

Nape amenusurika kifo katika ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Njia Nne Kilwa akiwa anatoka Dar kuelekea jimboni kwake.

Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Lindi alipata ajali hiyo baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa katika eneo la Nyangao mkoani Lindi.

Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake na ndiye alikuwa akiendesha gari hilo ambapo amepata majeraha madogo ila anaendelea vizuri.

Akizungumza na mtandao huu, Nape amesema: "Namshukuru Mungu nimetoka salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na michubuko ila ni mzima.

Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na 'air bag' nazo zimenisaidia."

Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo aliungana na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa na mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya shughuli hiyo alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.
 

0 comments:

Post a Comment