Tuesday 13 October 2015

#MICHEZO>>>Cristiano Ronaldo atunukiwa kiatu cha Dhahabu kwa Ufungaji Bora huko Ulaya na kuweka rekodi kwa kutwaa kwa mara ya nne.Fahamu zaidi hapa.

Cristiano Ronaldo msimu wa 2014/15, alifunga mabao 48 kwenye La Liga na kutwaa Buti ya Dhahabu kwa mara 3 akiwa na Real Madrid
Msimu wa 2007/08 akiwa na Manchester United alitwaa tena kiatu hicho baada ya kuwa mfungaji bora.
Hii ni mara ya kwanza katika Historia ya Miaka 47 ya Tuzo hii ya Buti ya Dhahabu kwa Mfungaji Bora wa Ligi za Ulaya kuichukua mara 4.
Ronaldo, ameifungia Real Jumla ya Mabao 323, na kufika Rekodi ya mabao mengi iliyokua imewekwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Raúl González Blanco aliyekua kaifungia timu hiyo mabao 323.

0 comments:

Post a Comment