Monday 5 October 2015

#YALIYOJIRI>>>Mgombea Ubunge ACT-Wazalendo amwombea kura Lowassa.Fahamu zaidi hapa.

Mgombea ubunge wa ACT - Wazalendo kwa Jimbo la Arusha Mjini, Estomih Malla jana baada ya kupanda jukwaani alimwombea kura za ndiyo mgombea urais Tanzania kupitia CHADEMA, Edward Lowassa.

Akihutubia mkutano wa kampeni uliokuwa na lengo la kunadi pia sera na kumwombea kura mgombea wa chama chake, Bi. Anna Mnghwira, katika Uwanja wa Stendi Kubwa, mkoani Arusha alisema:

“Jamani naombeni mtambue kuwa mimi ni msomi ambaye nina shahada (Hakuitaja ni ya nini), kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikitumia elimu yangu kwa faida ya familia yangu tu baada ya kufukuzwa udiwani na Chadema, sasa naombeni mnichague ili niitumie pia kuwatumikia kwa kuwaletea maendeleo yaliyoshindikana kupatikana kwa miaka mitano,”  “Mimi ni mkweli, nipeni ridhaa ya kuwaongoza na msisahau kumpa ridhaa ya kuwa rais mheshimiwa Edward Lowassa, naamini hamtajutia kura zenu,” alisema Malla.
Alipoulizwa baada ya kumaliza mkutano wake kwa nini amemnadi Lowassa badala ya mgombea urais wa chama chake, Malla hakutaka kujibu bali alipanda gari lake na kuondoka.
  • Habari hii imenukuliwa kutoka kwenye gazeti MWANANCHI

0 comments:

Post a Comment