Wednesday 7 October 2015

#MICHEZO>>>Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu waipa ushindi Taifa Stars leo.Fahamu zaidi hapa.

 Mbwana Samatta akipongezana na Thomas Ulimwengu baada ya goli la pili
 Thomas Ulimwengu akimiliki mpira mbele ya beki wa Malawi, Limbikani Mzava
 Kiungo wa Tanzania, Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Malawi, Mivale Gabeya

Mbwana Samatta akifunga baada kupata pasi kutoka kwa Thomas Ulimwengu na kumlamba chenga kipa wa Malawi, Simplex Nthala 


Taifa Stars ilianza mpira wa kasi na kupelekea ushindi wa mabao mawili 2 ambayo yamefungwa kipindi cha pili na wafungaji ni Samatta alianza kufunga dakika ya 18 baada ya kumlamba chenga kipa wa Malawi, Simplex Nthala, kufuatia  pasi ya Ulimwengu kutoka upande wa kulia.
 
Ulimwengu akafunga la pili dakika ya 22 akiuwahi mpira uliotemwa na kip Nthala kufuatia krosi ya beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali.
 
Ulichezeshwa na Hagi Yebarow Wiish aliyesaidiwa na Hamza hagi Abdi na Salah Omar Abubakar wote wa Somalia, ilikwenda kupumzika ikiwa tayari ina mabao hayo mawili kibindoni.

Kipa Ally Musafa Mtinge ‘Barthez’ aliokoa michomo miwili ya hatari ya Malawi kipindi cha kwanza, mmoja wa John Banda na mwingine wa Robin Ngalande.   
Kipindi cha pili, Malawi inayofundishwa na mzalendo pia, Ernest Mtawali ilibadilika na kukataa kuruhusu mabao zaidi.
Paka mpira unaisha Taifa Stars 2 na Marawi awajapata kitu.



0 comments:

Post a Comment