Sunday 4 October 2015

Tanzia Mch.Christopher Mtikila afariki kwa ajali ya gari.Fahamu zaidi hapa.

Kuna taarifa kwamba Mchungaji Christopher Mtikila amepata ajali ya gari mkoani Pwani alfajiri ya leo, taarifa zaidi tunasubiria kutoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani humo.

BREAKING NEWS:

 Baada ya mwandishi kuongea na Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema amefariki saa 12 kasorobo asubuhi katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.

Amesema gari lililokuwa limempakia lilikuwa linatokea Morogoro na kwamba walikuwa watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya.

Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya Tumbi.

                       Chanzo 
                                   JamiiForums                 

0 comments:

Post a Comment