Friday 2 October 2015

#YALIYOJIRI>>>Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwa Singida.Fahamu zaidi.

 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiombewa Dua na mmoja wa kiongozi wa dini mara baada ya kusimamishwa na Wananchi wa kijiji cha Puma (hawapo pichani),alipokuwa akielekea mkoani Singida mara baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara wa kampeni
 Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida jioni ya leo ,wakati akiwaomba  wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani. 

Dkt. Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inazisaidia taasisi mbalimbali  hasa za mashirika ya  dini ambazo zinaendesha hospitali  katika kupata vifaa, Ruzuku, na ajira kwa wafanyakazi ili   kuimarisha huduma  za kiafya  kwa jamii.
Sehemu ya umati wa Wakazi wa mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi kwenye mkutano wake wa mwisho kwa jioni ya leo,ambapo kesho anatarajia kuendelea na kampeni mkoani Singida na baadae kuhitimisha kampeni zake kwenye mkutano mkubwa ambao unatarajiwa kurushwa live na kituo cha Star TV

0 comments:

Post a Comment