Friday 9 October 2015

#YALIYOJIRI>>VIFAA VYA BVR VYANASWA VIKIANDIKISHA DAR.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Hofu ilitanda jana katika kiwanda cha MM Steel cha jijini Dar es Salaam, baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa mashine ya kusajili wapigakura kwa mfumo wa elektroniki (BVR) inatumika kuandikisha wafanyakazi katika kiwanda hicho. Kutokana na hofu hiyo, baadhi ya maofisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiongozwa na Mwanasheria wa chama hicho, John Mallya, Polisi na Tume Taifa ya Uchaguzi (Nec), walifika kiwandani humo na kufanya upekuzi ikiwamo kuondoka na baadhi ya vifaa vilivyokuwa vinatumika. Baada ya kukubaliana pande zote, vifaa hivyo ambavyo ni vya kuchukua alama za mikono, macho, scanner na kompyuta mpakato, vilichukuliwa na Polisi ili baadaye vikakabidhiwe Nec.

0 comments:

Post a Comment