Sunday 18 October 2015

#MICHEZO>>>Simba SC yang'ang'ania tatu bora baada ya ushindi wake.Fahamu zaidi hapa.

Timu ya Simba SC yang'ang'ania tatu bora baada ya  mechi ya sita ligi Tanzania bara ikiwa huko ugenini katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya imeifunga timu ya Mbeya City  kwa goli 0 – 1.
Goli la Simba lilifungwa katika kipindi cha kwanza dakika ya pili ya mchezo  na beki wa kimataifa Juuko Murdish. 

Goli hilo lilifanya hadi mpira unakwisha matokeo kuwa Mbeya City sifuli na moja Simba.
Akizungumza na waandushi wa habari baada ya mechi nahodha wa kikosi cha Simba Mussa Hassan Mgosi  alisema “tunamshuukuru Mungu kwa ushindi tulioupata leo tukiwa ugenini. Mchezo ulikuwa mgumu kwani sote tulicheza soka la ushindani mkubwa”.


 MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA HUKU SIMBA IKIONEKANA NAFASI YA TATU.
Pos Club P W D L GF GA GD PTS
1 Young Africans SC 6 5 1 0 14 2 12 16
2 Azam FC 6 5 1 0 10 3 7 16
3 Simba SC 6 5 0 1 8 3 5 15
4 Mtibwa Sugar FC 6 5 0 1 7 3 4 15
5 Stand United 7 4 0 3 7 4 3 12
6 Majimaji FC 7 3 1 3 4 4 0 10
7 Toto African 7 2 4 1 3 3 0 10
8 Tanzania Prisons 7 3 1 3 6 8 -2 10
9 Mwadui FC 6 2 2 2 3 2 1 8
10 JKT Mgambo 6 2 2 2 3 4 -1 8
11 Ndanda FC 6 1 3 2 4 5 -1 6
12 Kagera Sugar FC 6 1 2 3 2 7 -5 5
13 Mbeya City Council FC 7 1 1 5 5 7 -2 4
14 African Sports 6 1 0 5 1 7 -6 3
15 Coastal Union SC 7 0 3 4 0 6 -6 3
16 JKT Ruvu Stars 6 0 1 5 1 10 -9 1

0 comments:

Post a Comment