Saturday 3 October 2015

#YALIYOJIRI>>>Mwigulu Nchemba amkalibisha mgombea wa CCM John Pombe Magufuli mjini Kiomboi,wilayani Iramba.Fahamu zaidi hapa.

  Mgombea kupitia tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwigulu Nchemba kabla ya mkutano wa hadhara wa kampeni kuanza mjini Kiomboi,wilayani Iramba.
 Wananchi wakiwa wamefunga barabara wakizuia msafara wa Mgombea Urais Dkt John Pombe Magufuli katika kijiji cha sepuka na Ndago,wakati msafara huo ukielekea Iramba kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea Ubunge wa jimbo la Iramba Magharibi,Mwigulu Nchemba akiwahutubia wananchi wa Kiomboi mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni.
Ujenzi wa Daraja la Sibiti wilayani Mkalama likiwa katika hatua za mwisho kukamilika,Daraja hilo limeleta matumaini mapya kwa wakazi hao wa Mkalama,kwani wakati wa mvua ilikuwa ni kikwazo kikubwa kwao wakati wa kusafiri na hata kusafirisha mazao yao ya biashara.

0 comments:

Post a Comment