Monday 12 October 2015

#‎TANZIA‬>>>Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda amefariki dunia leo jioni nchini India.Fahamu zaidi hapa.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda amefariki dunia leo saa 10 jioni nchini India alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila amethibitisha taarifa hizo, na kusema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Apollo, New Delhi na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
Kwa mujibu wa kaka wa marehem Sadiki Kigoda aliyezungumza  siku chache zilizopita, alisema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo kushindwa kufanya kazi.

0 comments:

Post a Comment