Wednesday 16 November 2016

#Breaking>>>>Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu (IAA) ahukumiwa kwenda jela.Fahamu zaidi hapa.

Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu (IAA) cha Njiro mkoani Arusha, Profesa Johannes Monyo amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Sh milioni 1.5 baada ya kukutwa na kosa la kutoa ajira kwa Chacha Wambura kinyume cha sheria za utumishi wa umma.

Hukumu hiyo ilitolewa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Agustino Rwezile.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi Rwezile alisema mshitakiwa alikuwa anakabiliwa na makosa sita ambapo kosa la 1, 2, 3, 4 na 6 shitaka la ukiukwaji wa taratibu za utumishi wa umma kinyume cha kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Rwezile alisema kosa la 1, 2, 3, 4 mahakama imeona mshitakiwa hana hatia, lakini kosa la tano mshitakiwa aliloshitakiwa nalo la kutoa taarifa za uongo katika Bodi ya Chuo cha Uhasibu Njiro (IAA) ili kumpatia ajira Chacha Wambura, mahakama imemtia nalo hatiani.

“Mshitakiwa hakuwa na mamlaka ya kutoa ajira kwa Chacha kinyume cha utumishi wenye mamlaka hiyo, lakini yeye alimpa ajira ya kuwa Ofisa Rasilimali Watu na katika kipindi kifupi akampa kuwa Meneja wa Rasilimali Watu, kitendo ambacho ni kosa na hakuwa na kibali cha kufanya hivyo toka Utumishi,” alieleza Hakimu Rwezile.

Alisema mshitakiwa alitoa tangazo la ajira bila kusubiri majibu ya kibali cha Utumishi na akaendelea kutoa ajira wakati hana mamlaka ya kufanya hivyo na kusababisha Wambura kumpatia manufaa hivyo mahakama imemtia hatiani.

Katika kesi hiyo mshitakiwa alikuwa akishitakiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambao alikuwa akiwakilishwa na Mwanasheria wao, Violet Machary na walileta mashahidi wanne upande wa Jamhuri, huku mshitakiwa akisimama kujitetea mwenyewe.

Baada ya hukumu hiyo mshitakiwa alilipa faini na kujinasua kwenda kutumikia kifungo katika magereza ya Kisongo jijini Arusha.
– HABARILEO

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE
 

0 comments:

Post a Comment