Wednesday 23 November 2016

#YALIYOJIRI>>>>RUNGU LA RC MAKONDA LAMVAA MWENYEKITI WA SERIKALI ZA MITAA KWA TUHUMA ZA KUHUJUMU MAPATO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

MWENYEKITI WA MTAA WA GONGO LA MBOTO AKITIWA MBARONI NA JESHI LA [OLISI MARA BAADA YA AMRI YA RC MAKONDA 

Na Sosy

Mwenyekiti  wa Serikali ya Mtaa wa Gombo la Mboto Bakari Shingo atiwa mbaroni na jeshi la Polisi kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya  kuhusishwa na tuhuma za kukusanya mapato kwa kutumia risiti anazozichapisha mwenyewe kinyume na Halmashauri inavyoagiza, kutoitisha mikutano ya hadhara kwa muda mrefu na kushirikina na wahalifu.

tuhuma  hizo zimempelekea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye yupo kwenye ziara yake katika wilaya ya Ilala Pugu Kajiungeni, kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Salum Hamduni kumsweka rumande Mweyekiti huyo mpaka upelelezi utakapo kamilika.

Akitoa ushahidi kuhusu sakata hilo Mkazi wa Gongo la Mboto na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Pili Seif ameeleza kuwa hiyo imekuwa ni tabia ya mwenyekiti huyo kwa muda mrefu na taarifa zimefikishwa kwenye mamlaka husika ikiwemo kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema, Mkurugenzi Msongela Nitu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

0 comments:

Post a Comment