Friday 18 November 2016

#YALIYOJIRI>>>>Mamlaka ya Bandari Bandari yapokea boti mbili za kuegesha meli.Fahamu zaidi hapa.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepokea boti mbili za kisasa za kuhudumia meli kutoka China zitakazotumika katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga.
 Meneja Mawasiliano wa TPA, Janeth Ruzangi alisema ujio wa boti hizo zilizopolewa jana utasaidia kuongeza kasi ya utendaji kazi na ufanisi katika bandari hizo. 
Alisema ujio wa boti hizo ni sehemu ya mkakati wa TPA kuongeza vitendea kazi kwa upande wa majini na nchi kavu ili kuongeza kasi ya upakuaji na upakiaji wa mizigo kwa kiwango cha kimataifa na hivyo kuvutia wateja wengi. 
Nahodha Mkuu wa TPA, Kapteni Abdullah Mwingamno alisema boti ya tani 70 iliyopewa jina la Valeria Rugaihuruza itabaki Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudumia meli zinazoshusha mafuta katika Boya la SPM lililopo Mji Mwema, wakati nyingine inayoitwa Mwambani itapelekwa Bandari ya Tanga kwa ajili ya kuhudumia matishari. 
Boti ya MV Valeria Rugaihuruza imeundwa na ‘crane’ yake pamoja na boti nyingine ndogo mbili ndani yake kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi kwenye boya la mafuta. Boti ya MV Mwambani ina uwezo wa kuvuta tishari lenye uwezo wa kubeba tani 3,500 za mizigo.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

0 comments:

Post a Comment