Wednesday 16 November 2016

#MICHEZO>>>BAADA YA KUIBEBA ARGENTINA MESSI AONGOZA MGOMO.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Argentina bado inapambana kutafuta nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018 huko Urusi ambapo hadi sasa inashika nafasi ya tano ikiwa na alama 19 kwenye msimamo wa kanda ya Amerika ya Kusini. Alfajiri ya leo ilikuwa dimbani ilipoikaribisha Colombia na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Baada ya mchezo huo  nahodha wao Lionel Messi aliwaongoza wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina kususia kuongea na wanahabari baada ya kuwepo kwa tofauti kati yao huku sababu kubwa ikiwa ni kupinga shutuma dhidi ya uchezaji duni wa timu hiyo.

Messi mwenye miaka 29 ambaye pia katika mchezo huo alifunga bao moja na kusaidia kupatikana mengine mawili, alitangaza mgomo huo. Moja ya tuhuma zilizoripotiwa na kituo kimoja cha redio nchini humo ni kuhusu mshambuliaji Ezequiel Lavezzi kudaiwa kuvuta bangi wakati wa mazoezi lakini tuhuma hizo zilikanushwa.

Messi alisikika akisema “Tumebebeshwa tuhuma nyingi, Tumekosewa heshina sana na hatujasema lolote umefika muda sasa tuwe na maamuzi na haya ndio maaamuzi yetu,” alimaliza Messi akiwa na wenzake 25 kisha wakaondoka kwenye kikao cha wanahabari bila kuzungumza nao baada ya mechi.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE
 

0 comments:

Post a Comment