Wednesday 16 November 2016

#YALIYOJIRI>>>>LOWASSA AFICHUA SABABU YA KUTOONEKANA KATIKA MSIBA WA SITTA NA MUNGAI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu kutoonekana kwake kwenye misiba ya viongozi wawili wa zamani serikalini, Samuel Sitta na Joseph Mungai.
 

Sitta, aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, alifariki dunia Novemba 7, akiwa Ujerumani alikokwenda kutibiwa tezi dume na siku iliyofuata alifariki Mungai, aliyekuwa Waziri wa Elimu wa Serikali ya Awamu ya Tatu.
 
Gumzo kwenye mitandao ya kijamii lilikuwa ni kutoonekana kwa Lowassa, ambaye hivi sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
 
Lowassa alisema kuwa, kilichomkwamisha kufika kwenye misiba hiyo ni kuwa safarini Afrika Kusini alikokwenda kumuangalia mdogo wake, Bahati Lowassa aliyekuwa mgonjwa.
 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE
 

0 comments:

Post a Comment