Tuesday 15 November 2016

#MICHEZO>>>>MAWAZO YA HAJI MANARA KUHUSU TAIFA STARS.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Ninashudia aibu nyingine katika nchi za watu kwa kichapo kizito kutoka kwa Zimbabwe kwenye uwanja wa Taifa wa Harare, ni kipigo tulichokiandaa sisi wenyewe na ingekuwa ni miujiza walau kupata sare kule kwa Washona na Wandebele.

Wazimbabwe huku wakijua wanajiandaa na AFCON mapema mwakani walileta mziki kamili wa Profesionals wao karibia wote,huku akina sie tukiwa na pro wetu wawili Mbwana Samata na Elius Maguli wa FC Dhoufar ya kule Salala nchini Oman.

Wakati sisi tulikuwa na pro hao wenzetu wachezaji wanaocheza ligi ya kwao iliyobakisha mechi mbili ni wawili tu, yaani hapo ni kinyume nyume,na usisahau pro waliowaleta wanatamba huko ughaibuni kuanzia Belgium, Holland, Sweeden, Denmark hadi wale nyota wao wanaokipiga Keizer Chief na Mamelodi Sondowns ambao ndio mabingwa wa vilabu Afrika kwa sasa.

Nimesoma baadhi ya maandishi ya watanzania wenzangu baada ya kichapo cha Harare na kushangazwa kidogo, eti Mkwasa uwezo wake umeishia hapa, uuh lalaaa!! hizi lugha zimeanza kutawala sana siku hzi katika soka, naiona siku yangu nitakayoambiwa na washabiki wetu kuwa uwezo wangu katika usemaji wa klabu utakaposemwa umeishia hapa,kisa labda timu imefungwa na Orlando Pirates.   kwangu mimi hizi ni lugha za hovyo hovyo zinazoakisi uwezo wetu duni wa kupambanua mambo,nini kosa la Mkwasa katika hili?

Unategemea nini baada ya kuwakusanya wachezaji waliochoka na safari za ligi kuu inayobadilishwa ratiba kila uchwao, tunapojadili vitu tupendelee kuangalia uhalisia, eti kanuni zinaruhusu vilabu kupeleka wachezaji siku moja kabla kwa mechi za kirafiki huko.

Ni ujuha kufikiri tu kuwa hawa Local Players wetu wapo tayari kupambana na pro wa aina ya Musona wa Zimbabwe na wenzie,yampasa kocha walau apate siku tano angalau atrain na wachezaji wake, sikuona kwa nini ligi haikusimama wiki iliopita ili kumpa fursa kocha kdogo,nini kinalazimisha ratiba yetu kuwa na m’banano huu!!ktk hili bodi ya ligi ijipime upya.

Tuelewe hizi kanuni za FIFA ziliwalenga wachezaji na nchi za kiweledi, kwetu hazitatusaidia na lazima bodi na TFF wazingatie uwezo wa wachezaji wetu na ligi yenyewe, Ligi nyepesi yenye ushindani duni na maamuzi mabovu sambamba na tuhuma chungu mbovu.

Ligi inayotumia malando badala ya viwanja halisi vya ndiki,kisha makocha wa mitandaoni wanamlaumu Mkwasa, kocha mweledi na mwenye historia safi katika medani ya soka nchini, humfungi mtu ndugu mbongo kwa pro wawili au watatu labda utamuotea Somalia na Djibout, kwa sasa ukiingia hata na Comoro inabidi ubane ashua zako.

Wenzetu Zimbabwe wana kitengo maalum katika FA yao kuhakikisha kinapeleka pro wengi nje, sisi tunapiga porojo tu, Zimbabwe yenye uchumi wa hovyo lakini hakuna tuhuma za hovyo hovyo,wao kwao hapa Dar ni kama Dubai kwa wafanyabiashara wao, lakini uwanjani kwetu sisi ni kama wanacheza na watoto wa shule, kama yule abiria aliyemuuliza Samata nyie ni timu ya chuo?? hatuwezi kupiga hatua kama hatuwekezi kupata pro wengi, Never on Earth.

Iangalie Uganda leo ina pro wangapi?   wajisemee waunguja,ndio baaaasi tena,washatuacha!!! Ahhh nisiseme sana, hii ni nchi yangu na sina taifa lingine lolote, ila tuiunge mkono kila jitihada za kunusuru mpira toka TFF na vilabu vyetu na tusijtie kila mmoja kocha au mjuaji,vnginevyo Somalia wakimaliza vita watakuja kutufunga hapa hapa.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE
 

0 comments:

Post a Comment