Monday 14 November 2016

#MICHEZO>>>WAZIRI NAPE AMKABIDHI BENDERA MWAKILISHI WA TANZANIA MISS AFRIKA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Ndoto ya muda mrefu ya bara la Afrika kuwa mashindano ya ulimbwende imetimia ambapo kwa mwaka 2016 mashindano ya kwanza ya Miss Africa yanataraji kufanyika nchini Nigeria na kwa Tanzania, Miss Ilala 2016 na mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania 2016, Julitha Kabete anataraji kuwakilisha Tanzania katika mashindano hayo.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa bendera kwa ajili ya kwenda katika mashindano hayo ambayo yatafanyika Novemba, 26, Julitha Kabete amesema amejiandaa kwa ajili ya mashindano hayo na anaamini atafanya vizuri.

Kwa upande wa Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa, Nape Nnauye amesema ni nafasi ya kipekee Tanzania kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo na serikali ya awamu ya tano inataka kuhakikisha mashindano ya ulimbwende yanakuwa na thamani na yenye faida hivyo inamtakia safari njema na ipo nyuma yake kumpa msaada pindi unapohitajika.

“Tunataka mashindano ya Miss Tanzania ambaye anafaidika sio mshindi peke yake tumeona hapa huyu alikuwa mtu wa nne na amepata nafasi ya kuwakilisha nchi, tunafahamu mashindano ya Miss Tanzania yalikuwa yamefungiwa kufanyika ila sasa yamerudi vizuri na tutaendelea kuyaimarisha yawe bora na matarajio ya serikali ni kuona tunakuwa tunafanya vizuri na siku moja hata mshindi wa Miss World atoke Tanzania,” alisema Nape.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE
 

0 comments:

Post a Comment