Tuesday 15 November 2016

#MICHEZO>>>>DANIEL STURRIDGE ATAKA KUTIMKA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Mchezaji raha yake ni kucheza kila wiki mshahara unakuja baadae ili maisha yaende, unajua kwanini mara zote mchezaji anataka acheze kwa kuwa historia hutengenezwa na haiwezi kusahaulika kama ukiwa umefanya vizuri uwanjani.

Mshambuliaji wa Liverpool na Timu ya Taifa ya England Daniel Sturridge anafikiria kuondoka klabuni hapo mara baada ya maisha kumuendea kombo tangu ajiunge hapo akitokea Chelsea misimu 3 iliyopita.

Sturridge amekuwa mchezaji wa akiba mara zote akiwa nyuma ya washambuliaji Divork Origi pamoja na Firmino hivyo anakosa kiungia kikosi cha kwanza.

Kitaalam Sturridge amekuwa na majeraha sana tangu ajiunge hapo hivyo ni vizuri aondoke timu hiyo kwa ajili ya maisha yake ya baadae. Unaweza kuangalia tangu ajiunge na timu amecheza michezo  77 huku akifunga magoli 43.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE
 

0 comments:

Post a Comment