Wednesday 23 November 2016

#YALIYOJIRI>>>Mwathirika wa UKIMWI Aliyewanajisi Watoto 100 Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Miwil.Fahamu zaidi hapa.

Siku chache baada ya kuripotiwa taarifa za kukamatwa kwa mwanaume mmoja kutoka Malawi ambaye inadaiwa alikuwa akiwanajisi watoto wadogo wanaotajwa kufika 100 kwa maelezo kwamba anawasafisha na kufanya tambiko la kimila, Hatimaye amehukumiwa kwenda jela miaka miwili.

Hukumu hiyo imeonesha kutotenda haki kwa watoto hao kutokana na uchache wa miaka aliyofungwa mwanaume huyo. Tayari mashirika ya kutetea haki za binadamu na asasi za kupambana na maambukizi ya virusi vya HIV nchini Malawi zimekosoa hukumu hiyo

Michael Chipeta, wakili na mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini humo amekosoa hukumu hiyo na kusema kuwa kulikuwa na mapungufu mengi katika mchakato mzima wa kesi na hukumu dhidi ya mwathirika huyo wa virusi vya HIV, anayejulikana kama Eric Aniva mwenye umri wa miaka 45.

Eric Aniva alikiri kwamba amefanya ngono na wasichana wadogo kwa kulipwa fedha ambazo ni dola nne mpaka saba za Marekani kwa kuondoa usichana wa (kubikiri) kila mtoto mmoja, kwa imani kuwa ubikira ni mkosi na kwamba kitendo hicho kinawasafisha watoto hao pamoja na jamii hiyo.

Malawi ni katika nchi zenye maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi duniani.





Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

0 comments:

Post a Comment