Thursday 24 November 2016

#YALIYOJIRI>>>>Mikoa inayoongoza kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini Tanzania.Fahamu zaidi hapa.

Mikoa ya Tabora, Katavi na Rukwa imetajwa kuwa ni miongoni  mwa mikoa  10 inayoongoza kwa maambukizi  ya virusi vya ukimwi.

Hiyo ni  kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011/2012 za Taasisi ya Mkapa.

Taarifa hiyo  ilitolewa na Meneja Mradi wa TB na Ukimwi kutoka Taasisi ya Mkapa, Dkt. Happenes  Wilbroad     katika mafunzo ya siku moja  ya viongozi wa dini  yaliyofanyika   Nzega.

Alisema  mkoa unaoongoza kwa maambukizi ya VVU kati ya mikoa hiyo mitatu ni  Rukwa wenyeasilimia  6.2 ukifuatiwa na Katavi asilimia  5.2 na Tabora asilimia 5.1.

Dk. Wilbroad alisema Taasisi ya Mkapa  imeanza kuendesha  mafunzo ya kuhakikisha wananchi wanatambua na kuepuka maambukizi mapya.

Alisema    jitiahada mbalimbali za kudhibiti maambukizi  hayo zinapaswa kufanyika  kunusuru maisha ya  wakazi wa maeneo hayo.

Alitaja sababu zinazochangia   maambukizi kuwa ni pamoja na ndoa za utotoni, tohara za jadi na baadhi ya wananchi kutozingatia elimu ya Ukimwi   na kukithiri  imani potofu za ushirikina.




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

0 comments:

Post a Comment